Trump amteua tajiri mwenzake kuwa Waziri wa Mambo ya nje Marekani

by 00:38 0 maoni

Rais mteule nchini Marekani Donald Trump amemteua Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Exxon Mobil, Rex Tillerson kuwa  waziri wa mambo ya nje wa  Marekani.

Tillerson(64) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi ya Texas, Marekani .   Pia,   miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa duniani.

Tillerson anatajwa kuwa na uhusiano mwema na rais wa Urusi Vladimir Putin jambo ambalo limewatia wasiwasi wa wana Democrat na baadhi ya wa Republican

Uteuzi huo unahitaji kuthibitishwa na bunge la Senate.

Siku chache zilizopita ilibainika kuwa majasusi nchini Marekani wanaamini kuwa Urusi ilihusika na kushawishi ushindi wa Trump.

Unknown

Developer

Cras justo odio, dapibus ac facilisis in, egestas eget quam. Curabitur blandit tempus porttitor. Vivamus sagittis lacus vel augue laoreet rutrum faucibus dolor auctor.

0 maoni:

Chapisha Maoni