Desemba 10, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
zimetolewa tuzo kwa wasanii mbalimbali wa muziki na wa filamu kutoka
nje na ndani ya Tanzania.
Jumla ya tuzi 9 zilizotelewa kwa wasanii mbalimbali waliofanya vizuri
kwa mwaka 2016 ambapo tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa mtu aliyekuwa
na mchango mkubwa katika saanaa ya Tanzania na hivyo kufanya jumla ya
tuzo 10. Tuzo hii ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye.
Hapa chini ni orodha ya washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa usiku wa Desemba 10.
Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka- Safari ya Gwalu
Wimbo Bora wa Mwaka- Aje wa Ali Kiba
Video Bora ya Mwaka- Aje ya Ali Kiba
Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume- Salim Ahmed maarufu Gabo
Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike- Chuchu Hans
Kundi Bora la Muziki- Navy Kenzo
Mwanamuziki Bora Chipukizi- Amani Khamis maarufu Man Fongo
Tuzo ya Heshima- Dj Bonny Love
Mwanamuziki Bora wa Kike- Judith Wambura maarufu Lady JayDee
Mwanamuziki Bora wa Kiume- Ali Kiba
Mwanamuziki Ali Kiba ameweka rekodi katika tuzo hizi zilizotolewa kwa
mara ya kwanza baada ya kutwaa tuzo tatu ikiwa ni Video Bora ya Mwaka,
Wimbo Bora wa Mwaka, na Msanii Bora wa Kiume
Cras justo odio, dapibus ac facilisis in, egestas eget quam. Curabitur blandit tempus porttitor. Vivamus sagittis lacus vel augue laoreet rutrum faucibus dolor auctor.
0 maoni:
Chapisha Maoni