Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza nawafanyabiashara
ndogo ndogo marufu kama Machinga mtaa wa Kongo na kusikiliza kero zao
leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza wafanyabiashara wa
soko kuu la Kariakoo nakusikiliza kero zao leo jijiji Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa na viongozi mbalimbli akikagua soko la Kariakoo.
Ofisa
Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akifafanua jambo katika
mkutano wawafanyabiashara ndogo ndogo Machinga mtaa wa Kongo leo jijiji
Dar es Salaam.
Wafanyabiashara na wananchi wakimsikiliza mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAFANYABIASHARA
ndogo ndogo wa Kariakoo wametakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa na
viwanda vya ndani ili kukuza uchumi wa viwanda. Hayo ameyasema leo na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na
wafanyabiashara wandogo wandogo wa Kariakoo, amesema bidhaa
zinazozalishwa katika viwanda vya ndani zikipata soko nchi itapata
mapato pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu.
Amesema
serikali iko pamoja na wamachinga kuhakikisha wanafanya biashara kwa
mujibu wa sheria kwa kuuza vitu vyenye ubora na wakibaini kuwepo kwa
vitu ambavyo vinahatarisha maisha ya watanzania watachukuliwa hatua mara
moja.
Makonda
amesema ni marufuku wageni kutoka nje ya nchi kufanyabiashara ya
umachinga katika jiji la Dar es Salaam wao wanatakiwa kuleta utaalam tu.
Aidha amewaasa wamachinga kuwafichua wale ambao wanaweka rebo katika
bidhaa wakati hawazalishi wenyewe.
Makonda amesema katika maeneo ambayo wanafanyia kazi wamachinga kufuata sheria na kanuni zilizowekwa bila kuharibu utaratibu.
0 maoni:
Chapisha Maoni