Aliyekuwa
Mratibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, na Baadaye Mratibu wa Kampeni wa
ACT Wazalendo wakati wa uchaguzi Mkuu ulipita, Nixon Tugara akikabidhiwa
kadi ya CCM na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipoamua kuhamia
CCM wakati wa uzinduzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini
Dar es Salaam, leo.
Nixon
Tugara akifurahia kadi yake ya CCM baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la
Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo
Tugara
ambaye ni miongozi mwa watu waliosimamia ujenzi wa jengo hilo la
Kitegauchumi akizungumza yaliyomsibu hadi kuhamia CCM, kutoka ACT
Wazalendo na Chadema.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdultrahman Kinana akimshukuru Tugara kwa kuwa miongoni
mwa viongozi waliosaidia katika kufanikisha ujenzi wa jengo la
Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, ambalo
amelizindua leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakia Meghji.
Tugara akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea mwanachama mpya aliyejiunga na CCM kutokea Chadema, wakati wa hafla hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni