Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na wadau mbalimbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Sylivia Meku akielezea kwa wadau wa afya Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo, katikati ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Ally.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wadau mbalimbali wa Takwimu na Afya katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri
wa Afya na Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu,
amesema kuwa Utafiti unasema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria kwa
watoto chini ya mwaka mmoja kuwa malaria bado ni mojawapo ya magonjwa
yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto Nchini.
Ummy
amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa taarifa ya
utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na Malaria Tanzania ya mwaka 2015-16
(TDHS-MIS), katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
“
asilimia kubwa ya vifo vya watoto na akina mama wajawazito. Kiwango cha
maambukizi ya malaria kwa watoto chini ya mwaka mmoja kimeongezeka
kutoka asilimia 14 mwaka 2015/16 ukilinganisha na asilimia (9) ya mwaka
2010 kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid
Diagnostic Tests (RDT)” amesema Waziri Ummy.
Ameongeza
kuwa anatambua kwamba, suala hili limeshaanza kufanyiwa kazi ndani ya
Wizara na niwaombe wadau wote tushirikiane kwa pamoja katika kuendeleza
juhudi zilizopo za kuhakikisha Malaria inamalizwa hapa Tanzania. Hivyo
natambua Mpango wa Kudhibiti Malaria Tanzania (NMCP) upo katika
utekelezaji wa awamu nyingine ya kusambaza vyandarua katika Kaya za
Tanzania, tunategemea juhudi hizi na nyingine zinazofanywa na wadau
wengine zitachangia kupunguza kiwango cha Malaria hapa nchini.
Katika
hatua nyingine Waziri Ummy ameweza kuzungumzia tatizo la Mimba za utoto
kwa watoto wa kike walio na miaka 15 hadi 19 na kusema kuwa matokeo
yanaonesha kuwa asilimia 27 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19
wa mwaka 2015/16 wameshaanza kuzaa kulinganisha na asilimia 23 ya mwaka
2010.
Ameongeza
kuwa bado hii ni changamoto ambayo sote kwa pamoja tunatakiwa
kukabiliana nayo kwa kutoa elimu zaidi ili kupunguza kiwango hiki na
kuwezesha watoto wa kike waweze kupata muda wa kusoma na kujiendeleza
katika kujiandaa na maisha yao ya baadae. Hivyo, Serikali itaendelea
kutoa elimu juu ya madhara yanayoweza kutokea kwa wasichana kuzaa wakiwa
bado wadogo
0 maoni:
Chapisha Maoni