Waendesha Boda Boda wakisubir abiria
Waendesha
pikipiki za kusafirisha abiria (bodaboda) wilayani Nachingwea wameaswa
wasikubali kutumiwa na wanasiasa nakufanywa ngazi ya kufikia malengo yao
yakisiasa.
Wito huo
ulitolewa hivi karibuni na mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya
kiserikali ya kupambana na umasikini na utunzaji mazingira (APEC),
Respicius Timanywa.Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya usalama
barabarani iliyofanyika katika kijiji cha Chiola wilaya ya Nachingwea.
Timanywa
alisema madereva bodaboda ni kundi lenye nguvu katika jamii kutokana na
kuundwa na vijana. Hivyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa natabia ya
kuwalaghai ili wawaunge mkono kwa kuwataka washiriki kutekeleza vitendo
vya uvunjifu wa sheria. Ikiwamo kushiriki maandamano na mikutano isiyo
halali.
Mkurugenzi
huyo ambae taasisi yake inashugulika pia na kupunguza maafa kwa
waendesha pikipiki, alisema vijana hawana budi kukataa kutumika kufanya
vitendo vitakavyo vuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa maslahi ya
wanasiasa.
Badala yake wajiwekee malengo ya kufikia maendeleo kwakufanya kazi kwa juhudi na maarifa."Anzisheni
vikundi vya ujasiriamali na fungueni akaunti ili muweze kuungwa mkono
na serikali, muweze kukopeshwa kupitia fedha za mifuko ya vijana na
wanawake," alisisitiza Timanywa.
Aidha
alitoa wito kwa serikali iwatambue waendesha bodaboda kuwa nimiongoni
mwa watu wanaoweza kuchangia uchumi wa taifa kupitia kazi wanayofanya,
iwapo wataandaliwa mazingira mazuri ya kufanya kazi yao. Alibainisha
mchango wa vijana hao utatokana na kodi kupitia kazi wanayofanya. Hata
hivyo kwa mazingira ya sasa wanajiona kama wametengwa.
"Sasa
hivi hawana sehemu ya maalumu ya kuegesha pikipiki zao na hawana vituo,
wanapigwa na jua na mvua ikinyesha wanahangaika, serikali iwajengee
vituo wanaweza kuwa walipaji wazuri wa kodi," alisema Timanywa.Alisema
kunahaja ya vijana wanaohitimu mafunzo kupewa leseni haraka ili waanze
kulipa kodi na kuchangia pato la taifa. Hasa katika kipindi hiki ambacho
serikali ipo katika harakati kubwa za kuleta maendeleo ya nchi kupitia
ukusanyaji makini wa mapato na kuziba mianya wizi na ufisadi.
Mbali na
hayo, mkurugenzi huyo alitoa wito kwa serikali pitia jeshi la polisi
kuendelea kutoa ushirikiano na taasisi ili kuendelea kuwapa elimu
waendesha bodaboda. Kwani wasipopata elimu wataendelea kuwa chanzo cha
ajali nakusababisha madhara kwa taifa kutokana na kupoteza nguvu kazi.Akiongeza
kusema hata waendesha bodaboda watakuwa hawanufaiki na kazi hiyo.
Kwasababu sehemu kubwa ya mapato yao yatatumika kulipa faini kwa kukiuka
sheria za usalama barabarani.
Nae ofisa
tawala wa wilaya ya Nachingwea, Stephen Mbije, ambae alimuwakilisha
mkuu wa wilaya hiyo, aliwaasa vijana hao kujiunga na mfuko wa jamii wa
bima ya afya ili waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu. Huku
akiwaomba waanzishe vikundi vya ulinzi shiriki vya jamaii, ili
kukabilina uhalifu katika maeneo yao.
Kwa
upande wake, katibu wa washiriki hao, Deograsia Litimba, alisema licha
ya mafunzo hayo kuwafanya wazielewe sheria za usalama barabarani lakini
pia yamesababisha wabaini kuwa sababu ya mahusiano hafifu baina yao na
jeshi la polisi ni wao kutozitambua sheria.
Huku
akibainisha kuwa mafunzo hayo ambayo yalitolewa na APEC kwa kushirikiana
na jeshi hilo yamesababisha wawe na mahusiano mema nakuwa wanafamilia. Mafunzo
hayo ya wiki moja yalikuwa na washiriki 220 waliotoka katika za Mkoka,
Kipara Mtua, Kipara Mnero, Chiola, Marambo, Ruponda na Mnero Ngongo.
0 maoni:
Chapisha Maoni