Christian Bella: Ali Kiba na Diamamond hawapingiki

by 04:48 0 maoni

“Kwanini Diamond anapendwa? Diamond hapendwi si sababu ya kubeba vyuma tu, unaweza ukabeba vyuma na usipendwe vilevile. Angalia muziki wa Diamond kwanini unapendwa. Diamond anapendwa si kwaajili ya skendo kwasababu zile skendo pia huwa zinamuumizaga. Jamaa anatengeneza muziki mzuri, kubali ukatae,” alisema Bella kwenye mahojiano na Lake FM ya Mwanza.

“Mimi napenda anayefanya vizuri. Mimi kila nikitaka kutoa ngoma lazima napima ngoma ya Diamond, nitaangalia anaimba nini, kwanini watu wanampenda? Naangalia Alikiba, kwanini watu wanampenda, kaimba nini, naanza kupima ngoma zao. Halafu mimi natafuta, sio niimbe kama Diamond, sio nifanye kama Alikiba, natafuta njia pale katikati. Ukitaka baraka wakubali kwanza wanaokubalika,” alisisitiza Christian Bella

Unknown

Developer

Cras justo odio, dapibus ac facilisis in, egestas eget quam. Curabitur blandit tempus porttitor. Vivamus sagittis lacus vel augue laoreet rutrum faucibus dolor auctor.

0 maoni:

Chapisha Maoni